Sale!

Kuzitandua Tandabui

KSh500.00

Add to Wishlist
Add to Wishlist
Compare
  Ask a Question
Categories: ,

Description

Uturoho na Nyorita wameenda Mlima Bitoche na kutafuta vitovu kadhaa vya vinyonga. Watavitumia kuunda sumu kali kuwaua wananchi wa vijiji viwili walio kizungumkuti kwa wao
kuoana, kwa sababu hawa wawili wanatoka makabila tofauti.

“…kuna aina mbili za mvua ambazo watu hawatamani kunyeshewa. Ya kwanza ni mvua inayonyesha pamoja na mawe. Hii inaua mimea. Ya pili ni mvua ya jasho na mawe. Hii huwaua wahalifu wengi chini ya mwavuli wa mapigo ya kipopo. Mvua hiyo ya pili itatunyeshea kwa wingi leo…Damu inaenda kumwagika kama kwamba ni gilasi iliyopinduliwa…”

Je Uturoho na Nyorita, waliuliwa? Walifaulu kuoana? Ukabila nchini Rikafa uliisha?

Riwaya ya Kuzitandua Tandabui imeandikwa kwa utamu wa aina yake, kuelezea hadithi ya Uturoho na Nyorita wakithubutu kuondoa ukabila nchini Rikafa. Pata nakala yako ujue yote yaliyojiri.

Kuhusu Mwandishi wa Matini Chanzi

Mzaliwa 1997, Bonface Isaboke Nyamweya ni mwandishi Mkenya chipukizi. Amehitimu shahada ya falsa kutoka Chuo Kikuu cha Urbaniana, Roma. Sasa hivi, yeye ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Nairobi, anakosomea taaluma ya Sheria. Pia, ni mwanafunzi katika Catholic University of Eastern Africa anakosomea Uzamili katika Falsafa. Peeling the Cobwebs ndiyo riwaya yake ya
kwanza kuchapishwa kama matini chanzi kwa Kiingereza. Kupitia kwa mfasiri Kelvin Motuka, hii tafsiri imekamilika kwa lugha ya Kiswahili mufti kwa anwani: Kuzitandua tandabui .

Reviews

There are no reviews yet.

Only logged in customers who have purchased this product may leave a review.

No more offers for this product!

General Inquiries

There are no inquiries yet.