Kilio Cha Moyo

April 17, 2021 Off By Elias Bii

tmp-cam-822640927357560810.jpg

Maombi Ya Dhati Ya Moyo
Mwenyezi twakulilia, kwa dhati za roho zetu
Twakumbwa na kufungwa, kila dahari mwanetu
Mitetemeko dunia, tushikamane kukutu
Pamoja ‘shirikiana, tuondoe upumbavu.

Nzige barani Afrika, wamaliza kila jani
Ulimwengu korona, watisha kila wakati
Kung’ang’ana tunapaswa, nd’o masaibu tuepusheni
Tuungane kwa pamoja, tuondoe janga hili.

Wasemao wasemana, ‘likosea ni’ dunia?
Huku na kule korona, nzige pale na hapa
Ukosefu wa vyakula, turehemu Maulana
Kuchapo kuamshana, kazi tufanye pamoja.

Jalali tujalie, korona iwe mbali
Kuvamiwa na nzige, iwe jambo la mbali
Amani tuendeleze, tuweze ‘ishi vizuri
Kwako mola starehe, ipo maisha mazuri.
©Kiprobii