-
Genre:Riwaya
-
Originally Published:
-
Hardcover:
-
Language:,
Overview
Shaka Ya Maisha Na Hadithi Nyingine, ni diwani bambam ya Hadithi Fupi zizochirizwa na ‘wachawi’ waliobobea na wanaochipuka katika kilinge cha utanzu huu. Hadithi katika diwani hii, zimesukwa na kufumwa kwa nyuzi tofauti na kwa ubunifu wa hali ya juu.
Isitoshe, maudhui mbalimbali kama vile: Elimu, Malezi, Haki za kibinadamu, Unafiki, Umaskini, Ushirikina, Utamaduni, Usaliti, Tamaa, Uwajibikaji, Upendo, Mapenzi, Ndoa, Ufisadi, Siasa, Dini, jinsia, Nafasi ya mwanamke katika jamii, Uhalifu, Utabaka na Ubaguzi, Ukabila, Ureda na Anasa, Ugonjwa, Muamana na kadhalika yameakisiwa na kusawiriwa kwa ufasaha. Masuala ibuka yanayoathiri jamii mbalimbali katika mataifa ya kiafrika, yamepewa kipaumbele.
Mtindo, uumbaji wa wahusika, uchezaji wa maneno, udamisi na lugha iliyotumika ni viungo vitakayoibua ilhamu ya msomaji. Walengwa wa diwani hii ni wanafunzi wa shule za sekondari, vyuo vya ualimu pamwe na vyuo vikuu. Isitoshe, hadhira lengwa ya maashiki wengineo wa lugha ashirafu ya Kiswahili pia itanufaika pakubwa. Si watathmini, si wahariri, si wahakiki, si wachanganuzi.
BOOK DETAILS
- Hardcover:
- Publisher:
- Language: ,
- ISBN-10:
- Dimensions:
PREVIEW
Gallery Empty !
Average customer rating
There are no reviews yet.